Tetesi za Mastaa Ulaya: Gundogan afuata nyayo za Pep Guardiola, Liverpool yaingia sokoni kusaka kitasa wa Villa Ezri Konsa

Liverpool wanaendelea kumsoma mlinzi wa Aston Villa Ezri Konsa, 23, wakiwa na mpango wa kumsajili katika dirisha kubwa la usajili la mwezi Juni.

Liverpool, Manchester United, Manchester City na Tottenham zote kwa pamoja zinavutiwa kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Marekani na Schalke 04 Matthew Hoppe, 19.

Fowadi wa Ufaransa na Paris St-Germain Kylian Mbappe, 22, ameambiwa na klabu hiyo kuwa kama anahitaji kuondoka basi asubulie mpaka mkataba wake utakapo malizika mwishoni mwa mwezi Juni 2022.

Kiungo mshambuliaji wa Manchester City na Ujerumani IIlkay Gundogan, 30, amesema anahitaji kuwa mara baada ya kumaliza muda wake wa taaluma ya kusakata kabumbu ikimalizika.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares