Tetesi za Mastaa Ulaya: Haaland abakia ndotoni mwa Man United, Barca yajitutumua kwa Dani Olmo

Mshambuliaji wa kimataifa wa Norwei na Borussia Dortmund Erling Braut Haaland, 21, bado anaendelea kuwindwa na Manchester United ambapo inaelezwa kuwa mchezaji huyo anaweza kujiunga na Man United dirisha kubwa la mwaka 2022.

Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Manchester United Ed Woodward amepongezwa katika namna ambayo amefanya kukamilisha uhamisho wa staa wa Ureno Cristiano Ronaldo.
Kiungo mkabaji wa kimataifa wa Hispania Saul Niguez 26, atavalia jezi namba 17 kufuatia kukamilisha uhamisho wake wa kujiunga na Chelsea akitokea Atletico Madrid.
Barcelona watajaribu kumsajili nyota wa RB Leipzig na Hispania Dani Olmo, 23, ambapo dau la pauni milioni 50 lilikataliwa na Leipzig.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares