Tetesi za Mastaa Ulaya: Haaland aitaka Real Madrid, Rangnick huyo United

37

Mshambuliaji wa kimataifa wa Norwei na Borrusia Dortmund Erling Braut Haaland, 21, amesema angependelea kujiunga na Real Madrid endapo ataondoka katika klabu ya Dortmund.

Newcastle United wanaongoza mbio za kuwania saini ya mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa na Fc Barcelona Ousmane Dembele 24, ambaye pia anawindwa na Manchester United katika dirisha kubwa la usajili mwezi Juni 2022.

Manchester United iko kwenye hatua za mwisho kukamilisha uhamisho wa kocha na Mkurugenzi wa Ufundi Ralf Rangnick, 63, kwa ajili ya kurithi mikoba ya Ole Gunnar Solskjaer aliyetimuliwa klabuni hapo baada ya matokeo ya kipigo kizito cha goli 4-1 kutoka kwa Watford. United inaendelea kuhangaika kibali cha kazi baada ya kumalizana na Lokomotiv Moscow.

Kiungo mkabaji wa Leeds United na timu ya taifa ya England Kalvin Phillips, 25, amesema atabakia Elland Road licha ya ushawishi wa Manchester United.

Author: Bruce Amani