Tetesi za Mastaa Ulaya: Harry Kane agomea kurudi kambini Spurs, Ofa ya Man United kutua Real Madrid

Manchester United wanategemea kutuma ofa rasmi kwenda kwa beki wa kati wa Real Madrid Raphael Varane, 28, wiki ijayo, hata hivyo haitegemei kufika kiasi cha pauni milioni 50 ambacho klabu ya Madrid inahitaji kwa mchezaji huyo.

 

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa Varane amekuwa akihitajika na klabu nyingine Ulaya kama Paris St-Germain na Chelsea mbali na Manchester United wenyewe.

 

Wachezaji wenza wa Harry Kane, 27, wanaamini kuwa mchezaji huyo hataripoti kambini kujiandaa na msimu ujao wa EPL kutokana na kuhitaji kushinikiza dili la kuondoka Tottenham Hotspur, Manchester City na Chelsea zinahusishwa naye.

 

Fenerbahce wako kwenye mazungumzo na West Ham United kwa ajili ya kumsajili winga wa Ukraine Andriy Yarmolenko, 31.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares