Tetesi za Mastaa Ulaya: Havertz ashauriwa kwenda Dortmund na sio Liverpool, Karius bado yupo yupo Liverpool

Kiungo mshambuliaji wa Bayer Leverkusen na Ujerumani Kai Havertz, 20, ameambiwa aachane na dili la kujiunga na Liverpool badala yake ajiunge na Borrusia Dortmund hayo yamesemwa na mchezaji wa zamani wa Ujerumani Jens Nowotny.

Juventus huenda wakawaweka sokoni wachezaji wao wakubwa ili kupunguza gharama za kuendesha timu kiungo wa Bosnia Miralem Pjanic, 30, na Gonzalo Higuain, 32, wanaweza kuwa wahanga wa utaratibu huo.

Barcelona wapo mbioni kumsajili mshambuliaji wa Inter Milan Lautaro Martinez 22, na Pjanic 30, wa Juventus.

Manchester United wamerudisha majeshi ya kumwania mlinzi wa Napoli na Senegal Kalidou Koulibaly, 28, licha ya Liverpool pia kumtaka kitasa huyo.

Mlinda mlango wa Liverpool Loris Karius, 26, haitarejea mazoezi hivi karibuni ambapo alishakatisha mkataba na klabu ya Besiktas.

Wolves wamemuongezea mkataba wa mwaka mmoja golikipa wao John Ruddy, 33, ili aendelee kukitumikia kikosi hicho.

Kocha wa zamani wa Tottenham Hotspurs Mauricio Pochettino anaweza kujiunga na timu yoyote ile endapo itajitokeza, siku za usoni Newcastle United wamekuwa wakihusishwa kumsajili.

Author: Bruce Amani