Tetesi za Mastaa Ulaya: Ighalo kuendelea kusalia Manchester United, Bakayoko atafuta timu ya kuchezea

Manchester United wanataka kurefusha mkataba wa mkopo wa mshambuliaji wa Kinegeria Odion Ighalo 30, ambaye ametokea Shanghai Shenhua ya China.

Arsenal wana matumaini ya kupata saini ya mlinzi wa Paris Saint – Germain Layvin Kurzawa, 27, baada kuwepo uwezekano mdogo wa kujiunga na miamba ya Catalunya, FC Barcelona.

Liverpool, Southampton na RB Leipzig wako vitani kuwania saini ya winga wa Werder Bremen Milot Rashica, 23, ambaye kandarasi yake inamalizika mwishoni mwa mwezi Juni.

Kiungo mshambuliaji wa Chelsea Tiemoue Bakayoko, ambaye yuko kwa mkopo Monaco anatamani kurudi AC Milan ambako alichezea msimu wa 2018/19 kwa mkopo pia. 

Manchester City wanaandaa Euro 32m kwa ajili ya kumsajili mlinzi wa Marseille Boubacar Kamara, 20.

Roma wanaitaka Arsenal walipe nusu ya mshahara (£180000) wa mshambuliaji raia wa Armenia Henrikh Mkhitaryan endapo wanahitaji kweli mchezaji huyo asajiliwe moja kwa moja klabuni Roma.

Hata hivyo The Gunners wapo kwenye mpango wa kumvuta Emirates beki wa RB Leipzig Dayot Upamecano, 21, Tottenham na Manchester United wanavutiwa kumsajili mlinzi huyo pia.

Kufuatia muda wa kuwa kwa mkopo kwa mlinda mlango Loris karius, 26, Besiktas kuvunjwa, mchezaji huyo amepanga kurudi Liverpool ili akamalizie miaka miwili iliyosalia kwenye mikataba.

Huenda kocha Jurgen Klopp angekuwa kocha wa Mexico 2015 baada ya kushawishiwa kwa muda mrefu na taifa hilo kabla ya Klopp kuchukua maamuzi ya kwenda nyumbani kwa Liverpool Anfield.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends