Tetesi za Mastaa Ulaya: James Rodriguez kung’oka Everton, Chelsea yamuwinda mlinzi wa Bayern Munich

Kiungo mshambuliaji wa Everton na raia wa Colombia James Rodriguez, 29, anafikiria kuondoka klabuni hapo licha ya kujiunga miamba hiyo ya Goodison Park mwishoni mwa msimu uliopita kutokea Real Madrid.

Manchester City wametuma ofa bab kubwa kwa nyota wa Barcelona Lionel Messi, 33, ya pauni milioni 430. Inaelezwa kuwa ofa hiyo ni ndogo kulinganisha na ile Man City waliituma kwa nyota huyo ya pauni milioni 600 miezi sita iliyopita, mkataba wa Messi unamalizika mwishoni mwa mwezi Juni.

Chelsea wanahitaji kumsajili beki wa kati wa Bayern Munich raia wa Ujerumani Niklas Sule, 25.

Real Madrid wameendelea kuwa kipaumbele cha kumsajili winga wa kimataifa wa Ufaransa na klabu ya Paris St-Germain Kylian Mbappe, 22.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares