Tetesi za Mastaa Ulaya: Jesus wa Man City kuwa mbadala wa Ronaldo Juve

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola anahitaji kumsajili kiungo mshambuliaji wa Aston Villa na timu ya taifa ya England Jack Grealish 25.

Inaelezwa kuwa Manchester United iko kwenye hatua za mwisho kukamilisha uhamisho wa winga wa Borrusia Dortmund Jadon Sancho, 21, ambapo kiasi cha pauni milioni 80 kutumika.

Staa wa Ureno Cristiano Ronaldo 36, anaendelea kuangalia uwezekano wa kuondoka Juventus licha ya kuwa yupo kwenye mazungumzo na klabu hiyo juu ya mkataba mpya.

Kama Ronaldo ataondoka Juve basi mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil Gabriel Jesus, 24, anatajwa kuwa kwenye orodha ya watakaoziba nafasi.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares