Tetesi za Mastaa Ulaya: Juventus yaipiku Real Madrid kwa Erling Braut Haaland, Gonzalo Higuain kurudi tena EPL?

Arsenal wameanza mazungumzo na kiungo mshambuliaji wa Barcelona Philippe Coutinho, 27. Wababe wa Ujerumani Bayern Munich ambao walipewa kipaumbele cha kumsajili hawako tayari kumchukua Coutinho kwa dau la £105m.

Paris St-Germain wako kwenye mazungumzo na Arsenal juu ya kumsajili mshambuliaji wa Gabon Pierre Emerick Aubameyang 30, kwa dau la £34.

Mshambuliaji wa Juventus Gonzalo Higuain, 32, anaweza kurudi tena EPL baada ya kipindi chake cha mkopo ndani ya Chelsea kutoridhisha kutokana kushindwa kuonyesha makeke, Newcastle United na Wolves wameonyesha nia ya kumsajili.

Strika wa RB Leipzig Timo Werner, 24, amekuwa akihusishwa zaidi kujiunga na Liverpool lakini kiungo wa zamani wa Manchester United Owen Hargreaves anaamini mshambuliaji huyo anastahiri zaidi kutua Old Trafford.

Mshambuliaji wa Wolves Raul Jimenez, 29 ambaye anafikia dau la £57m, yupo kwenye rada katika timu ya Manchester United, Arsenal na Real Madrid.

Juventus wanahitaji kumsajili mfumania nyavu wa Borrusia Dortmund na kuzipiku Real Madrid na Paris Saint Germain juu ya huduma ya Erling Braut Haaland, 19.

Barcelona wako tayari kupunguza gharama za kumuuza winga wake Ousmane Dembele, 23, ambaye hivi sasa anatolewa kwa £37m. Klabu hiyo ya Catalunya ilimchukua kwa £137m miaka mitatu kutoka Borrusia Dortmund.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends