Tetesi za Mastaa Ulaya: Kane aingia anga za PSG, Mourinho akalia kuti kavu Tottenham

Kocha Mauricio Pochettino wa Paris St-Germain amewaambia matajiri wa Jiji la Paris kuwa anahitaji kuungana tena na mshambuliaji wa kimataifa wa England Harry Kane, 27, kama tu winga wa Kifaransa Kylian Mbappe na Neymar Jr wataondoka klabuni hapo.

Bosi wa Leicester Brendan Rodgers anaongoza mbio za makocha wanaotajwa kuchukua mikoba ya kocha Jose Mourinho katika klabu ya Tottenham Hotspur.

Mshambuliaji wa kimataifa wa Norwei Erling Braut Haaland, 20, anahitaji pauni milioni 78 ili kuondoka Borussia Dortmund mwishoni mwa msimu huu, Real Madrid wanatajwa kuwania saini yake.

Barcelona wamejumuisha majina ya washambuliaji wawili watakaokuwa kwenye rada ya klabu hiyo kwenye dirisha kubwa la usajili la mwezi Juni, majina ya wachezaji hao ni Erling Braut Haaland na Sergio Kun Aguero.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares