Tetesi za Mastaa Ulaya: ‘Kijeba’ Adama Traore ahusishwa kutua Manchester United, Arsenal wajifariji kwa Moussa Diaby

Winga wa Manchester City Leroy Sane, 24, amesema havutiwi na tetesi zinazomhusisha kwenda kwa wapinzani wa City Liverpool, lakini siku za karibuni amekuwa akihusishwa kujiunga na Bayern Munich.

Mshambuliaji wa Borussia Dortmund Erling Braut Haaland, 19, aliipiga chini ofa ya Juventus mwezi Januari baada ya miamba Hao kutaka kumsajili na kumuweka katika timu ya vijana chini ya umri wa miaka 23.

Manchester United ni miongoni mwa timu zinazowania saini ya staa wa Wolverhampton Wanderers Adama Traore, 22, hata hivyo upinzani ni mkubwa kwani Liverpool na Manchester City zote zinasaka saini ya kijeba huyo mwenye mianguko ya kipekee.

Arsenal wana matumaini ya kumsajili winga wa Bayer Leverkusen na Ufaransa Moussa Diaby, 20, kinda huyo wa zamani wa PSG alitoa asisti 2 katika ushindi wa kikosi chake dhidi ya Werder Bremen mchezo wa ligi kuu Ujerumani Bundesliga.

Chelsea wanaongoza mbio za kunasa saini ya mlinzi wa Barcelona Xavier Mbuyamba, 18, wakala wa mchezaji huyo amethibitisha juu ya The Blues kuhitaji huduma ya kinda huyo.

Author: Bruce Amani