Tetesi za Mastaa Ulaya: Kipa wa Man United Henderson atishia kung’oka klabuni hapo, Nagelsmann kuchukua mikoba ya Mourinho

Mlinda mlango wa England na klabu ya Manchester United Dean Henderson, 23, atatafuta klabu nyingine mwishoni mwa msimu huu endapo hata hakikishiwa nafasi ya kwanza kwenye kikosi cha timu hiyo.

Kocha wa RB Leipzig Julian Nagelsmann ameanza kuhusishwa kutua kunako klabu ya Tottenham Hotspur na anapangwa kurithi mikoba ya kocha mwenye maneno mengi Jose Mourinho.

Juventus na Inter Milan wameingia kwenye vita ya kuwania saini ya mshambuliaji wa kati wa Manchester City na raia wa Argentina Sergio Kun Aguero 32 ambaye anahitajika na Barcelona na Real Madrid.

Paris St-Germain wako tayari kuanzisha upya mpango wa kumsajili beki wa kulia wa Arsenal na Hispania Hector Bellerin, 25, ambaye amekuwa akiwindwa kwa udi na uvumba na Barcelona.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares