Tetesi za Mastaa Ulaya: Kocha Pochettino ataka Mbappe kubakia PSG, Man United wamuachia Paul Pogba

324

Manchester United watamuuza kiungo mshambuliaji wao raia wa Ufaransa Paul Pogba 27 katika dirisha kubwa la usajili la mwezi Juni.

Manchester United hawana uhakika kama dili la kumpata winga wa Borrusia Dortmund Jadon Sancho 20 litafanikiwa mwishoni mwa mwezi Juni baada ya Ole Gunnar Solskjaer kuonyesha matumaini ya kumpata mshambuliaji Erling Braut Haaland.

Bosi mpya wa Paris St-Germain Mauricio Pochettino anamatumaini winga wa klabu hiyo Kylian Mbappe 22 ataendelea kubakia klabuni hapo licha ya kuhusishwa kujiunga na Liverpool sambamba na Real Madrid.
Atalanta wako tayari kumuachia winga wa Ivory Coast Amad Diallo, 18, kwenda Manchester United kumalizia mechi ya msimu huu.

Author: Bruce Amani