Tetesi za Mastaa Ulaya: Kocha Zidane awaaga wachezaji wake Real Madrid, Messi kutua Man City

Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane amewaambia wachezaji wake kuwa ataachana na timu hiyo mwishoni mwa msimu huu.
Bosi wa Everton Carlo Ancelotti na yule wa zamani wa Juventus Massimiliano Allegri ni miongoni mwa majina yanayotajwa kuchukua nafasi ya Zidane ndani ya Real Madrid kama ataondoka klabuni hapo.
Manchester City wameambiwa wanaweza kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina Lionel Messi 33 endapo klabu hiyo itakuwa na uwezo wa kumlipa pauni 500,000 kwa wiki baada ya makato ya kodi.
Manchester United wanahitaji kumuongeza mkataba mpya kiungo mshambuliaji wake raia wa Ufaransa Paul Pogba, 28, hata hivyo wanahofu na mahitaji makubwa ya fedha kutoka kwa Wakala Mino Raiola.
Winga wa Lyon na Uholanzi Memphis Depay, 27, yuko njia panda juu ya kufanya maamuzi ya kubakia Lyon au kujiunga na miamba ya soka la Hispania Fc Barcelona.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares