Tetesi za Mastaa Ulaya: Kocha Zinedine awasiliana na wakala wa Paul Pogba, Inter Milan kujipima kwa Alexandre Lacazette wa Arsenal

Chelsea wamemwekea kipaumbele cha kumsajili beki wa pembeni wa Leicester City Ben Chilwell, 23, ambaye anapatikana kwa dau la £85m, ingawa watakabiliwa na ushindani kutoka kwa Arsenal.

Meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane amezungumza na wakala wa Paul Pogba, 27, wa Manchester United juu ya hatima yake, ambapo wakala huyo amemthibitishia kuwa nyota huyo anavutiwa bado kuchezea Real Madrid hasa chini ya kocha Zinedine.

Manchester United wanatazamia kumvuta winga wa Valez Sarsfield Thiago Almada, 19, kama mbadala wa winga wa Borrusia Dortmund Jadon Sancho ambaye dili lake lina washindani wengi hivyo ni ngumu kufanikiwa kumsajili.

Inter Milan watajaribu kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Alexandre Lacazette, 29, mpango wa Inter Milan ni kutafuta mbadala wa Lautaro Martinez, 22, ambaye anawindwa na Barcelona.

Tottenham imempa mlinzi wa pembeni Danny Rose, 29, ruhusa ya kuendelea kutumika katika klabu ya Newcastle United kwa mkopo.

EPL imeviambia vilabu kuwa mechi zisizozidi nne kwa kila klabu zitachezwa katika viwanja vya ugenini, hiyo ina maanisha kuwa kuna uwezekano Liverpool ikatwaa ubingwa wa EPL nje ya dimba la Anfield.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends