Tetesi za Mastaa Ulaya: Koulibaly atajwa Everton, Nicolo Barella kwenye rada za Liverpool

Beki wa England na Atletico Madrid Kieran Trippier, 30, anatamani kurejea katika Ligi Kuu ya England huku klabu ya Manchester United ikionyesha nia ya kumsajili.

Everton wamefungua mazungumzo ya kumsajili beki wa kati wa Napoli na timu ya taifa ya Senegal Kalidou Koulibaly, 30, ambaye inaelezwa ni kipaumbele cha kocha Rafa Benitez.
Liverpool wameandaa kiasi cha pauni milioni 60 kwa ajili ya kumsajili kiungo wa Inter Milan na Italia Nicolo Barella, 24.
West Ham wako mbioni kukamilisha uhamisho wa golikipa wa Paris St-Germain na Ufaransa Alphonse Areola, 28.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares