Tetesi za Mastaa Ulaya: Leicester City yajipima kwa Adam Lallana wa Liverpool, Gareth Bale bado yupo yupo Real Madrid

Leicester wamefanya mazungumzo ya awali ya kukamilisha dili la kumsajili kiungo mshambuliaji wa Liverpool Adama Lallana, 32, kiungo huyo wa Uingereza atakuwa nje ya kandarasi mwezi Juni Anfield.

Real Madrid hawajapokea ofa yoyote ya kumhitaji mchezaji wake raia wa Wales Gareth Bale, 30, winga huyo huenda akaendelea kukaa klabuni hapo kwa mwaka mwingine.

Manchester United na Newcastle wanavutiwa kumsajili kinda wa Uruguayi Facundo Pellistri, 18, ambaye anakipiga kunako Penarol.

Galatasaray wanahitaji kumsajili winga wa Bournemouth Ryan Fraser, 26, winga huyo amekuwa akitajwa kwenda katika klabu ya Arsenal na Tottenham.

Everton wanafanya mazungumzo hivi sasa na mlinzi wa pembeni wa Ufaransa Djibril Sidibe, 27, juu ya kuongeza muda wa mkopo baada ya ligi kuendelea mwezi Juni, beki huyo ametokea klabu mama ya AS Monaco.

Shanghai Shenhua wamerahisisha vikwazo vyao juu ya kumhitaji mshambuliaji wao raia wa Nigeria ambaye anakipiga kunako klabu ya Manchester United kwa mkopo Odion Ighalo juu ya kusogeza mbele kandarasi yake.

Paris St-Germain wako mbioni kukamilisha uhamisho wa moja kwa moja kwa mshambuliaji wa Argentina Mario Icardi, 27. Strika huyo yupo kwa mkopo PSG kutokea Inter Milan kandarasi yake inatamatika Mei 31.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends