Tetesi za Mastaa Ulaya: Leicester City yashitukia mbinu za Man United na Liverpool

109

Leicester City wako hatua nzuri kwenye mazungumzo na kiungo mshambuliaji wa timu hiyo na England Harvey Barnes, 23, ya kumuongeza mkataba mpya, Liverpool na Manchester United zinatajwa kuwania saini yake.

Liverpool wanatajwa kuanza kufikiria uwezekano wa kumchukua kocha wa Rangers ambaye pia ni nahodha wa zamani wa timu hiyo Steven Gerrard kuwa mrithi wa mikoba ya kocha Jurgen Klopp kama nafasi itatokea.

Manchester United watatakiwa kumlipa kiasi cha pauni milioni 1.7 endapo watashindwa kumuongeza mkataba wa mwaka mmoja nyota wao Edinson Cavani, 34.

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amesema mahusiano yake na Wakala Mino Raiola hayamzuii yeye (Pep) kumsajili mshambuliaji wa Norwei na klabu ya Borrusia Dortmund Erling Braut Haaland, 20.

Author: Bruce Amani