Tetesi za Mastaa Ulaya: Lewandowski ampa ushauri Haaland timu sahihi ya kuichezea, Chelsea yamkosa straika Mertenes wa Napoli

Kiungo mshambuliaji wa Manchester City David Silva, 34, kandarasi yake ndani ya klabu hiyo inamalizika Juni 30 lakini yuko tayari kuongeza mkataba wa kuhakikisha anamaliza mechi zilizosalia msimu huu

Manchester United wanavutiwa kumsajili winga wa Schalke 04 ya Ujerumani Rabbi Matondo 19, lakini usajili huo utatokea endapo watashindwa kumvuta Jadon Sancho, 20.

Huenda Chelsea wakashindwa kumpata mshambuliaji wa Napoli ya Serie A Dries Mertens baada ya staa huyo kuonyesha nia ya kuendelea kusalia katika klabu yake, licha ya Inter Milan kutamani kumsajili strika huyo raia wa Ubeligiji.

Mshambuliaji wa Bayern Munich na Poland Robert Lewandowski, 31, amemshauri mshambuliaji wa Borrusia Dortmund Erling Braut Haaland, 19, ambaye anahusishwa kujiunga na Manchester United na Real Madrid kuwa ni bora aendelee kubakia hapo ili akuze zaidi kipaji chake.

Wakala wa kiungo mshambuliaji wa Brazil na Barcelona Philippe Coutinho, 27, amesema hajafanya mazungumzo na klabu yoyote ile kwa ajili ya kuhitaji huduma ya staa huyo ambaye yuko kwa mkopo Bayern Munich. 

Leeds United wataweza kumshawishi mlinzi wa Tottenham Hotspur Juan Foryth, 22, ya kujiunga na timu hiyo endapo watafanikiwa kupanda daraja kuingia EPL.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends