Tetesi za Mastaa Ulaya: Liverpool haijakata tamaa kwa Ibrahima Konate

Liverpool bado wanampango wa kumsajili beki wa kati wa RB Leipzig na Ufaransa Ibrahima Konate 21, licha ya kiwango cha fedha hitajika kuonekana kikubwa tofauti na matarajio ya Majogoo wa Jiji la Merseyside.

Mazungumzo ya mkataba mpya kwa mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil Neymar Jr, 29, ndani ya PSG yanaendelea ambapo nyota huyo amesema wamefikia hatua nzuri mpaka sasa.

Meneja wa Leicester City Brendan Rodgers amesema havutiwi na kuwa kocha wa kikosi cha Tottenham Hotspur kama mbadala wa Jose Mourinho aliyetimuliwa kufuatia matokeo mabovu.

Barcelona wanaendelea na mazungumzo na kiungo mkabaji wa Uholanzi na Juventus Matthijs de Ligt, 21.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares