Tetesi za Mastaa Ulaya; Liverpool, Spurs zabaniwa kwa Adama Traore, Dybala abakia mfalme Juventus

Wolves wameandaa kiasi cha pauni 120,000 kwa wiki kwa ajili ya Adama Traore 25, fedha ambazo zitamfanya nyota huyo wa kimataifa wa Hispania kuwa mchezaji anayelipwa zaidi klabu hapo.

Real Madrid waliandaa mikataba saba ya kushauriana na winga wa Paris St-Germain Kylian Mbappe 22, wakikusudia kumsajili katika siku ya mwisho ya dirisha kubwa la usajili, hata hivyo bado wanamatumaini ya kumsajili baada ya kandarasi yake kumalizika 2022.

Eduardo Camavinga, 18, nyota wa Ufaransa inaelezwa kuwa alikubali kujiunga na Real Madrid akitokea Rennes licha ya kitita kirefu cha PSG ambacho kilitengwa kwa kinda huyo.

Juventus wameanza ujenzi wa timu hiyo kumzunguka nyota wa Argentina Paulo Dybala, 27, hii ni baada ya kumruhusu Ronaldo kujiunga na Manchester United.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares