Tetesi za Mastaa Ulaya: Liverpool wamekusudia kujiimarisha eneo la ulinzi kwa kumchukua Kalidou Koulibaly wa Napoli, Coutinho bado kwenye rada za Newcastle United

229

Newcastle watatumia £70m kwa ajili ya kumvuta kiungo mshambuliaji wa Barcelona na Brazil Philippe Coutinho kama watafanikiwa kuichukua timu hiyo. Coutinho hivi sasa yuko Bayern Munich kwa mkopo.

Mabwenyenye wa Newcastle watafikiria kumchukua mlinzi wa Napoli na Senegal Kalidou Koulibaly, 28, mlinzi huyo anategemea kuondoka klabuni mwishoni mwa mwezi Juni.

Hata hivyo, Kalidou Koulibaly huyo anawindwa na Liverpool.

Borussia Dortmund wanatarajia winga wao raia wa England Jadon Sancho, 20, atasalia klabuni licha ya kuendelea kutamani kwenda Manchester United.

Chelsea, Manchester United na Tottenham wanawania saini ya kiungo wa Lazio Sergej Milinkovic-Savic, ambapo kiungo huyo raia wa Ubeligiji anapatikana kwa dau la £80m.

Meneja wa Henrikh Mkhitaryan amesema kuwa taarifa za Arsenal kutaka kumuuza staa wao raia wa Armenia mwenye miaka 31 sio sahihi.

Kiungo mshambuliaji wa Barcelona Ivan Rakitic, 32, amesema hajafikiria kuondoka klabuni hapo hata baada ya kumalizika kwa kandarasi 2021.

Author: Bruce Amani