Tetesi za Mastaa Ulaya: Liverpool yaenda kwa Roma kusaka saini ya Pellegrini aliyeisumbua Man United, Man City yasaka saini ya Niguez

Aliyekuwa kocha wa Wolves Nuno Espirito Santo ameingia njia panda ya kutua katika klabu ya Crystal Palace kufuatia klabu ya Everton kuelezwa kuwa wako njiani kutuma ofa.
Atletico Madrid wametuma ofa kwa kiungo mshambuliaji wa Ureno na Manchester City Bernardo Silva, 26, hata hivyo kuna uwezekano wa kufanya mabadilishano na kiungo Saul Niguez.
Liverpool imetuma ofa ya pauni milioni 25.8 kwa klabu ya Roma yenye uhitaji wa kiungo na nahodha wa klabu hiyo Lorenzo Pellegrini, 24, kuwa mbadala wa kiungo wa Uholanzi Georginio Wijnaldum 30, aliyebwaga manyanga klabuni hapo.
Juventus imeanza mchakato wa kumchukua mlinzi wa kulia wa Arsenal Hector Bellerin ambapo kiungo mshambuliaji wa Wales Aaron Ramsey anaweza kurudi tena The Gunners.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares