Tetesi za Mastaa Ulaya: Liverpool yapeleka donge nono kwa Kalidou Koulibaly, Raul Jimenez wa Wolves awindwa na Juventus

365

Chelsea wanategemea kuhamisha nguvu za kumsajili beki wa kushoto kwa Paris Saint-Germain ambaye atakuwa huru mwishoni mwa msimu huu Layvin Kurzawa, 27, endapo watashindwa kumsajili beki wa Leicester City Ben Chilwell, 23, ambaye huenda akaendelea kusalia klabuni hapo.

Barcelona wamefungua mazungumzo juu ya mkataba mpya kwa staa wao Lionel Messi, 32, timu hiyo inakusudia kumpa kandarasi ya miaka miwili, mchezaji huyo anatimiza miaka 33 Jumatano.

Juventus ipo tayari kumtoa mlinzi wake na timu ya taifa ya Italia Daniele Rugani, 25, na winga Federico Bernardeschi, 26, kwa ajili ya kumpata mshambuliaji wa Mexico na Wolverhampton Raul Jimenez, 29.

Liverpool wametoa £54m kwa ajili ya kumnasa beki wa Napoli na Senegal Kalidou Koulibaly. Kisiki huyo mwenye umri wa miaka 29 anawindwa pia na Manchester United na Chelsea. 

Roma wamemuahidi mlinzi wa Tottenham na Ubeligiji Jan Vertonghen, 33, kandarasi ya miaka miwili, na kipengele cha mwaka mmoja wa ziada, atakamaliza miaka hiyo miwili.

Everton ipo tayari kuanza rada za kumwania mlinzi wa Real Valladolid Mohammed Salisu, 21. Beki huyo raia wa Ghana anakipengele kinachomruhusu kuondoka klabuni hapo kwa pauni milioni 10. 8, Manchester United na Southampton ni miongoni mwa timu ambazo zinahitaji huduma ya mlinzi huyo.

Author: Bruce Amani