Tetesi za Mastaa Ulaya: Mafahali wawili Sancho, Greenwood washindwa kuishi Zizi moja

312

Manchesterer United imeweka wazi kuwa winga wa Borussia Dortmund Jadon Sancho 21, sio kipaumbele tena cha usajili kwa klabu hiyo, hii ni baada ya kuibuka kwa kinda wa kiingereza pia Mason Greenwood ambaye amekuwa na wakati mzuri chini ya Ole Gunnar Solskjaer.
Arsenal wanamtaja kiungo mshambuliaji wa Kifaransa Eduardo Camavinga, 18, ambaye anachezea klabu ya Rennes ya Ligue 1 kama chaguo la kwanza kwake.
Hata hivyo, The gunners wanaendelea kuangalia uwezekano wa kumsajili kiungo wa Switzerland na Borussia Monchengladbach Denis Zakaria, 24.
Wakala wa kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa England na Aston Villa Jack Grealish 25, amesema vilabu vingi vimekuwa wakihitaji huduma ya Bosi wake lakini bado havijafikia makubaliano.
AC Milan wamesema wanahitaji kumsajili beki wa kati wa Chelsea na England Fikayo Tomori, 23, kwa kandarasi ya moja kwa moja baada ya kutumika klabuni hapo kwa mkopo wa msimu mzima.

Author: Bruce Amani