Tetesi za Mastaa Ulaya: Man City kumkosa Jack Grealish, Raiola atangatanga na Pogba

Klabu ya Aaston villa imepanga kuanza mazungumzo na kiungo mshambuliaji Jack Grealish 25, wiki ijayo ili kumpatia mkataba mpya ambao utamfanya kuendelea kubakia klabuni hapo kwa muda na kuzima matumaini ya Manchester City.
Hata hivyo, Mabingwa hao wa EPL wanaendelea na mazungumzo na wawakilishi wa mchezaji pamoja na klabu ili kumchukua kabla ya kupewa kandarasi mpya ndani ya Villa Park.
Wakala wa Paul Pogba, 28, Mino Raiola amesema kama klabu ya Manchester United haitatenga fedha nzuri yuko tayari kumpeleka bosi wake katika timu ya Liverpool.
Mlinda mlango wa Manchester City na Brazil Ederson, 27, yuko kwenye hatua za mwishoni kuongeza kandarasi mpya ya kuendelea kukitumikia kikosi hicho, kandarasi ya miaka mitatu imeandaliwa.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares