Tetesi za Mastaa Ulaya: Man City wajitoa kwa Messi, Arsenal warudi tena kwa Zaha wa Crystal Palace

West Ham watafanya liwekezanalo kuhakikisha wanakamili uhamisho wa kiungo mshambuliaji wa Manchester United Jesse Lingard 28 ambaye sasa anakipiga klabuni hapo kwa mkopo.

Manchester United wanahitaji ada ya pauni milioni 30 kwa Jesse Lingard kujiunga na Wagonga Nyundo wa London West Ham United.

Arsenal wameamusha tena matamanio ya kumsajili winga hatari wa Crystal Palace na Ivory Coast Wilfred Zaha, 28.

Manchester City wanaendelea na mazungumzo ya mikataba mipya na nyota wake wawili Phil Foden, 20, na Raheem Sterling, 26, hii ni baada ya kukamilisha uingiwaji wa mkataba mpya kwa Kelvin de Bruyne hadi 2025.

Vinara wa EPL Manchester City hawatafanya jaribio la kumnunua nyota wa kimataifa wa Argentina Lionel Messi 33 mpaka mchezaji huyo aonyesha nia ya kuondoka.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares