Tetesi za Mastaa Ulaya: Man City yaanza na Haaland, Liverpool huru kwa Chamberlain

Wakala wa mshambuliaji wa kimataifa wa Norwei na Borussia Dortmund Erling Braut Haaland, 21, Mino Raiola anatarajia kufanya mazungumzo na Manchester City kuangalia uwezekano wa kuhamia klabu hiyo.

Winga wa England Raheem Sterling, 26, amesema bado anahitaji kupambana kujihakikishia namba kwenye kikosi cha kwanza cha kocha Pep Guardiola ndani ya Man City.

Liverpool wako tayari kumuachia kiungo mshambuliaji raia wa England Alex Oxlade-Chamberlain, 28, lakini watamuachia kwa kiasi cha fedha sahihi.

Kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa England na Manchester City Phil Foden, 21, yuko kwenye mazungumzo ya mwishoni kuongeza mkataba mpya klabuni hapo.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends