Tetesi za Mastaa Ulaya: Man United na Pogba wayajenga, faili la Kane lafika kwa mabosi wa Juventus

Juventus wanavutiwa kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa England na Tottenham Hotspur Harry Kane 27, dau kubwa kwa mchezaji huyo linatajwa kuwa sababu zinazofaya hilo kutotokea, ingawa Kane mwenyewe aliongea kuwa anahitaji kuondoka klabuni hapo.

Manchester United wameanza mazungumzo na wawakilishi wa kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa Paul Pogba 28, kwa ajili ya mkataba mpya.

Kiungo mshambuliaji wa Manchester City na Ujerumani Ilkay Gundogan, 30, anatazamia kuona kama Barcelona wataweza kutuma ofa ya kumhitaji kabla ya kufanya maamuzi ya kubakia Man City kwa kuongeza kandarasi mpya au la.

Hata hivyo, Mabingwa hao wa EPL hawana mpango wa kumuuza kiungo huyo wa zamani wa Borrusia Dortmund.

Kocha wa West Ham David Moyes, 58, yuko njia panda na mkataba mpya wa miaka mitatu kuendelea kusalia ndani ya Wagonga Nyundo wa London baada Everton kuanza kumshawishi.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares