Tetesi za Mastaa Ulaya: Man United yasaka saini ya Federico Valverde kutoka Real Madrid

Manchester United wako kwenye mchakato wa kumsajili kiungo mkabaji wa Real Madrid na Uruguayi Federico Valverde mwenye umri wa miaka 22.

Everton watajaribu kwa mara nyingine tena kumsajili kiungo mshambuliaji wa zamani wa Paris St-Germain na sasa Juventus na Ufaransa Adrien Rabiot, 25, katika majira ya kiangazi ya dirisha kubwa la usajili.

Mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa na Paris St-Germain Kylian Mbappe, ambaye mkataba wake ndani ya PSG unamalizika mwishoni mwa mwezi Juni mwaka 2022 amesema anafuraha na maisha ya Ligue 1 ingawa hilo halitoi uwezekano wa kuwa anaweza kuondoka klabuni hapo.

Mlinzi wa kati wa Bayern Munich na Austria David Alaba, 28, anahitaji kuondoka klabuni hapo na kujiunga na miamba ya soka la Ulaya Real Madrid katika majira ya joto.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares