Tetesi za Mastaa Ulaya: Man United yatoa ofa ya mkataba mnono kumfunga Pogba Old Trafford

Mtendaji Mkuu wa Paris St-Germain Leonardo amesema anaamini mshambuliaji wa timu hiyo Neymar Jr, 29, ambaye ni raia wa Brazil atabakia klabuni hapo.

Manchester United wataanza upya tena kufanya mazungumzo na kiungo mshambuliaji wa Ufaransa Paul Pogba 28, huku ikiwa imeboresha mkataba wake, na sasa mshahara wake utakuwa pauni 400,000 kwa wiki.

Kocha wa West Ham David Moyes amesema klabu hiyo itaingia sokoni katika kuwania saini ya mshambuliaji wa Chelsea na England Tammy Abraham, 23, dau lake linafikia pauni milioni 45.

West Brom imeanza mazungumzo na kocha Sam Allardyce juu ya kumuongeza mkataba mpya kwani kandarasi ya sasa inafikia ukomo pale ambapo West Bromwich watashuka daraja.

Leicester City wameingia kwenye vita ya kuwania saini ya kiungo wa Ufaransa ambaye anakipiga kunako klabu ya Lille Boubakary Soumare, 22, hata hivyo itapambana na Manchester United ambayo pia inahitaji saini yake.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares