Tetesi za Mastaa Ulaya: Man Utd kutuma pauni milioni 90 kwa Sancho wiki ijayo, Odoi ataka kutolewa nje ya Stamford Bridge

Manchester United watatuma ofa ya mwisho wiki ijayo ya pauni milioni 90 kwenda kwa winga wa Borrusia Dortmund Jadon Sancho, 20, ikiwa ni sehemu ya ushawishi wa winga huyo kutua Old Trafford.

Arsenal wameonyesha nia ya kumhitaji kiungo mkabaji wa Chelsea na Italia Jorginho, 28.

Everton ni miongoni mwa timu ambazo zinamhitaji kipa wa Manchester United na Argentina Sergio Romero, 33, ambapo presha inaongezeka kwa mlinda mlango namba moja wa vijana hao wa Toffees Jordan Pickford.

Lucas Torreira, 24, bado hajaamua aende wapi kati ya Atletico Madrid na Torino kwani klabu zote zinania ya kumsajili kiungo huyo raia wa Uruguay.

Beki wa kushoto wa Porto Alex Telles anaamini bei wanayohitaji Porto ya Euro milioni 20 kwa Manchester United haina uhalisia kwani atakuwa mchezaji huru mwishoni mwa msimu ujao.

Manchester City wamekanusha taarifa iliyokuwa ikidai kuwa klabu hiyo imetuma ofa ya pauni milioni 78 kwa beki wa Atletico Madrid Jose Gimenez, 25 sio ya kweli.

Monaco wameonyesha matumaini ya kumsajili kiungo mshambuliaji wa Tottenham Hotspur na England Dele Alli, 24,

Wakati huo huo, Paris St-Germain wameandaa donge nono kwa kiungo Alli huyo ambaye amekosa nafasi mbele ya jeuri Jose Mourinho.

Fowadi kinda wa Chelsea na England Callum Hudson-Odoi, 19, analazimisha kuondoka kwa mkopo Stamford Bridge kwenda kwingineko ili apate nafasi nzuri ya kucheza.

Kiungo mshambuliaji wa Barcelona na Brazil Philippe Coutinho, 28, anaweza kujiunga na Arsenal kwa mkopo kabla dirisha hili kubwa la usajili kufungwa.

Author: Bruce Amani