Tetesi za Mastaa Ulaya: Manchester City kupinga adhabu ya kutoshiriki Uefa, Sancho kutimukia Real Madrid

Real Madrid wanavutiwa kumsajili winga wa Borrusia Dortmund Jadon Sancho, 20, mwenye uraia wa England.

Juventus wanafikiria kuishawishi Barcelona juu ya kumsaini winga wa Ufaransa Ousmane Dembele, 23, kwa mkopo msimu ujao.

Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer ana matumaini ya kukuza dau la usajili kwa kuwauza mastaa wake watatu beki wa Argentina Marcos Rojo, 30, mshambuliaji wa Chile Alexis Sanchez, 31, na Chris Smalling 30, kutokana na janga la virusi vya Corona.

Winga wa Bournemouth Ryan Fraser, 26, ataondoka mwishoni mwa msimu huu bure kutokana na kandarasi yake kutamatika ambapo inaelezwa atakuwa dili kubwa kwa vilabu vya EPL.

Paris St-Germain wanahitaji donge nono la Euro milioni 175 kutoka Barcelona kama kweli wanahitaji kumsajili tena mshambuliaji wa Kibrazil Neymar, 28.

Watazamaji watapewa chaguo la kusikia kelele za mashabiki zisizo za kweli (feki) katika michuano ya ligi pale itakaporudi ili kuongeza hamasa kwa waangaliaji watakao kuwa nyumbani.

Kocha na mkongwe wa soka Diego Maradona, 59, ataendelea kusalia katika klabu ya Gimnasia y Esgrima mpaka mwishoni mwa msimu wa 2020-2021 baada ya kocha huyo kuongeza mkataba mpya.

Mashabiki wa Manchester City wamepanga kuonyesha hasira zao kwa Shirikisho la Soka Ulaya siku ya Ijumaa juu ya kupinga ‘kifungo cha kikatili’ cha kutoshiriki mashindano ya Uefa.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends