Tetesi za Mastaa Ulaya: Manchester City wajiweka sawa kumvuta Messi Etihad

Klabu ya Manchester kwenye nafasi nzuri ya kumsajili staa wa Barcelona na Argentina Lionel Messi, 33, kufuatia klabu hiyo kuingia kwenye kandarasi na kocha Pep Guardiola ikiwa sehemu ya matakwa ya Messi.

Manchester United watatuma ofa kwenda kwa kiungo wa Rennes Edouard Camavinga, 18, lakini watatakiwa kushindana na matajiri wa Ufaransa Paris St-Germain.

Baadhi ya vilabu vya EPL vimeonyesha nia ya kumsajili mlinzi wa Real Madrid na Hispania Sergio Ramos, 34, ambapo mlinzi huyo yuko kwenye mwaka wa mwisho wa mkataba wake.

Hata hivyo, Real Madrid watamsajili beki wa Bayern Munich David Alaba, 28, bila kujali kama Ramos ataondoka au atasalia klabuni hapo.

Everton watazamia kutuma ofa kwa Manchester United kuhitaji huduma ya winga wa United Daniel James 23 ambapo kiberenge huyo amekosa nafasi ya kutosha Old Trafford.

Author: Bruce Amani