Tetesi za Mastaa Ulaya: Messi akubali kubakia Barca kwa masharti maalumu, Tammy Abraham sokoni darajani

Mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina Lionel Messi 33, ataongeza mkataba mpya wa kuendelea kukitumikia kikosi cha Barcelona lakini kwa masharti maalumu ya kumleta strika Erling Braut Haaland wa Borussia Dortmund.

Manchester City wako tayari kumuachia winga wa England Raheem Sterling 26 katika majira ya kiangazi huku mbadala wake akitajwa kuwa ni kiungo mshambuliaji wa Aston Villa Jack Grealish, 25.

Chelsea wanajaribu kuingilia kati dili la Barcelona la kumsajili kiungo wa Juventus Adrien Rabiot, 26, ambapo nyota huyo wa Ufaransa anapatikana kwa dau la pauni milioni 17 pekee.

Leicester wameungana na Aston Villa na Wolves kwenye kinyang’anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa England Tammy Abraham 23.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares