Tetesi za Mastaa Ulaya: Mkataba Mpya Wagonga mwamba Liverpool na Henderson, Man City yahamia kwa Nuno Mendes

Bado haieleweki hatima ya kiungo mkabaji wa England na Liverpool Jordan Henderson kufuatia mazungumzo ya kandarasi mpya kwa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 31 kushindwa kufikia mwafaka.

 

Manchester City wanavutiwa kumsajili beki wa kushoto wa Sporting Lisbon na Ureno Nuno Mendes, 19, lakini hawako tayari kutoa kiasi cha pauni 50.

 

Atletico Madrid imesisitiza kuwa beki wao na England Kieran Trippier, 30, hauzwi kama ambavyo klabu ya Manchester United imekuwa ikuhusishwa kumsajili mlinzi huyo wa zamani wa Tottenham Hotspur.

 

Beki wa kati wa Real Madrid na Ufaransa Raphael Varane 28, amesema kuwa mazungumzo ya masuala binafsi haitakuwa tatizo.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares