Tetesi za Mastaa Ulaya: Mo Salah kumwaga wino Liverpool, Pochettino kutua Manchester

Inaelezwa kuwa baadhi ya wachezaji wa Paris St-Germain wanajua kuwa kocha wa timu hiyo Mauricio Pochettino ataondoka klabuni hapo na kujiunga na Manchester United ambapo kocha Zinedine Zidane anategemewa kuenda Ufaransa.

Manchester United watalazimika kutoa kiasi cha pauni milioni 8.4 sawa na Euro milioni 10 kwa Paris St-Germain kama fidia ya kuvunja mkataba kwa kocha huyo mwenye umri wa miaka 49.

Kocha wa Sevilla Julen Lopetegui, 55, ameongeza kasi ya kujiweka sokoni kuwania nafasi iliyoachwa wazi ya kocha Ole Gunnar Solskjaer ndani ya Old Trafford.

Winga wa kimataifa wa Misri Mohamed Salah 29, yuko mbioni kumwaga wino wa kuendelea kukitumikia kikosi cha Majogoo wa Jiji la Merseyside Liverpool ambapo mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea Anaingia kwenye mwaka wa mwisho wa kandarasi yake Anfield.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends