Tetesi za Mastaa Ulaya: Mrithi wa Solskjaer kitendawili Ulaya

Kocha wa Paris St-Germain ambaye ni raia wa Argentina Mauricio Pochettino anatajwa kuwa kwenye kipaumbele cha kwanza katika kazi ya kuinoa Manchester United baada ya klabu hiyo kumfuta kazi ya ukocha Ole Gunnar Solskjaer, makocha wengine ni kocha wa Ajax Erik ten Hag na Zinedine Zidane.

Manchester United imefanya mazungumzo tena na kocha wa Leicester City Brendan Rodgers, ambapo kumpata kwake lazima ulipe fidia kiasi cha pauni milioni 8.

Wakala wa Kireno Jorge Mendes anaendelea kupambana kuhakikisha kocha wa Sevilla na kocha wa zamani wa Real Madrid Julen Lopetegui anachukua urithi wa Ole Gunnar Solskjaer Manchester United. Mkataba wa mhispania huyo unamalizika mwishoni mwa msimu wa 2024.

Kocha wa Hispania Luis Enrique amekanusha vikali taarifa za kuhusishwa kujiunga na Manchester United.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends