Tetesi za Mastaa Ulaya: Mwenyekiti wa Spurs amcharukia Mourinho, hatima ya Giroud mikononi mwa Tuchel

Mwenyekiti wa klabu ya Tottenham Hotspur Daniel Levy anahitaji kusubili mpaka mwishoni mwa msimu huu kujua hatima ya kocha Jose Mourinho ambaye bado hajawa na mwendelezo mzuri wa matokeo.

Nyota na mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina na Manchester City amesema hana uhakika kama msimu huu utakuwa wa mwisho kuwa kwenye uzi wa klabu vinara Man City.

Mshambuliaji wa Barcelona na Argentina Lionel Messi 33, bado hajafanya maamuzi sehemu atakayokuwa msimu ujao, wawakilishi wake wanaendelea na mazungumzo na klabu nyingine barani Ulaya.

Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amethibitisha kuwa atakuwa na mazungumzo na mshambuliaji wa timu hiyo Edinson Cavani, 34, juu ya kurefusha mkataba wake.

Kocha Mkuu wa Chelsea Thomas Tuchel amesisitiza kuwa “ni mapema mno” kufanya maamuzi ya kumbakiza au kumtema mshambuliaji wa Kifaransa Olivier Giroud, 34.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares