Tetesi za Mastaa Ulaya: Mwenyekiti wa Spurs Levy kumbakiza Gareth Bale, Sancho sokoni

Leicester City na Everton ni miongoni mwa timu zinazowania saini ya mshambuliaji wa Brentford Ivan Toney, 25.

Mwenyekiti wa klabu ya Tottenham Daniel Levy amesema kocha ajaye klabuni hapo atapewa kipaumbele cha kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid ambaye anakipiga kwa mkopo Gareth Bale 31.

Borussia Dortmund wamepunguza dau la kumuuza mshambuliaji wao raia wa England Jadon Sancho 21, kwa sasa anauzwa kwa pauni milioni 87 kutoka milioni 100, Manchester United na Liverpool zinahitaji saini yake.

Klabu ya Newcastle United na ile ya Atalanta zimeonyesha nia ya kumhitaji mlinzi wa Uholanzi Vitesse Arnhem, 22, ambaye anachezea kikosi cha Rangers.

Wakala wa Robert Lewandowski, Pini Zahavi amepanga kushinikiza mkataba mpya wa Bosi wake wenye thamani zaidi, strika huyo matata anaelekea mwishoni mwa mkataba wake lakini anahitajika na vilabu vya PSG, Juventus.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares