Tetesi za Mastaa Ulaya: Newcastle United yawania saini ya Mbappe, Man United yatapatapa kumpata mrithi wa Solskjaer

Newcastle United imejitosa katika vita ya kuwania saini ya winga wa kimataifa wa Ufaransa na Paris St-Germain Kylian Mbappe 22, ambaye mkataba wake unafikia tamati mwishoni mwa msimu huu.

Winga wa Morocco Hakim Ziyech, 28, na fowadi wa Ujerumani Timo Werner, 25, wote wakikipiga Chelsea wameibuka kama wachezaji mbadala wa Raheem Sterling 26, kutua Man City katika dirisha dogo la usajili la mwezi Januari 2022.

Maombi ya Manchester United yakumuomba kocha Mauricio Pochettino kuwa mrithi wa Ole Gunnar Solskjaer yamepigwa chini na Paris St-Germain.

Kwa sasa makocha wanaohusishwa kwenye dili la United mi kocha wa zamani wa Borrusia Dortmund Lucien Favre, kocha wa zamani wa Lyon Rudi Garcia na Paulo Fonseca kocha wa zamani wa Roma.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends