Tetesi za Mastaa Ulaya: Neymar Jr ajifunga PSG hadi 2026, Haaland ni “keki ya moto” kwa vigogo Ulaya

Nyota wa Brazil Neymar, 29, ameingia kandarasi ya awali ya mpaka mwaka 2026 na matajiri Paris St-Germain ambapo mkakati wa klabu ni kuhakikisha inampa mkataba kama huo wa winga matata Kylian Mbappe, 22.

Imebainika kuwa timu itakayomchukua mshambuliaji wa Borussia Dortmund Erling Braut Haaland itaigharimu fedha za ziada kiasi cha pauni milioni 34 (Euro 40) ambazo Wakala Mino Raiola na Baba mzazi wa Haaland Alfa Inge wanahitaji kama sehemu ya kukamilisha uhamisho huo.

Haaland Ana kipengele kinachohitaji timu inayomchukua kutoa kitita cha pauni milioni 64, hata hivyo Dortmund wanahitaji kumpa kandarasi ya mwaka mmoja kuendelea kuwepo klabuni hapo ingawa mchezaji huyo akihitaji kuondoka.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Norwei Erling Braut Haaland 20 amekuwa akihitajika na kocha wa Barcelona Ronald Koeman ambaye amesema maamuzi ya kumsajili yatatolewa na Rais wa klabu hiyo Joan Laporta.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares