Tetesi za Mastaa Ulaya: Neymar kutundika daluga baada ya Qatar 2022, Arsenal yajitupa kwa Chamberlain

Arsenal wanafikiria uwezekano wa kumrudisha kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa England na Liverpool Alex Oxlade-Chamberlain, 28, ambaye alidumu klabuni hapo kwa miaka sita kabla ya kutimukia Anfield 2017.

Makamu Rais wa Barcelona Rafael Yuste amesema itakuwa vigumu kwa klabu hiyo kuingia sokoni kuwania saini ya mshambuliaji wa Borussia Dortmund Erling Braut Haaland 21, ambaye amekuwa akihusishwa kujiunga na Real Madrid na Manchester City.
Mshambuliaji wa Brazil Neymar Jr, 29, amesema fainali za Kombe la Dunia Qatar 2022 zitakuwa za mwisho kucheza akisema baada ya hapo hadhani kama atakuwa na ngumu kuhimili ushindani.
Mambwenyenye wapya wa Newcastle United wanafikiria kumchukua kocha wa Leicester City Brendan Rodgers na kumkacha kocha wa sasa klabuni hapo Steve Bruce.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends