Tetesi za Mastaa Ulaya: Nyota wa PSG Idrissa Gueye akataa kujiunga na Newcastle United

Leicester City wanavutiwa kumsajili kiungo mkabaji wa Watford na England Nathaniel Chalobah, 26, katika siku ya mwisho ya usajili.

Liverpool wamefanya mazungumzo ya awali na klabu ya Marseille juu ya kumhitaji beki wa kati wa kimataifa wa Croatia Duje Caleta Car, 24.

Kiungo mkabaji wa klabu matajiri wa Ufaransa Paris St-Germain ambaye ni raia wa Senegal Idrissa Gueye, 31, amekataa ofa ya Newcastle United ambayo ilikuwa inamhitaji nyota huyo kwa mkopo.

Beki wa Manchester United Marcos Rojo, 30, atajiunga na klabu ya Boca Juniors kama mchezaji huru baada ya Mashetani Wekundu kusitisha mkataba wake mwishoni mwa mwaka Jana.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares