Tetesi za Mastaa Ulaya: Odion Ighalo aiomba Shanghai Shenhua kuendelea kuitumikia Manchester United, Liverpool yajipangia bei ya Timo Werner

41

Liverpool wanavutiwa kumsajili winga wa Wolves raia wa Hispania Adama Traore, 24, tayari Bosi wa Liverpool Jurgen Klopp imeripotiwa kaanza mazungumzo binafsi ya winga huyo mwenye mwili mkubwa.

Mshambuliaji wa Nigeria Odion Ighalo, 30, amefanya maombi maalumu ya kuomba kusogezwa kwa mkataba wake na Manchester United kutoka katika klabu ya Shanghai Shenhua.

Mlinzi wa kati wa Arsenal David Luiz anaweza akasepa mwishoni mwa msimu huu kwani kandarasi inamalizika mwezi ujao na hakuna mazungumzo yanayoendelea.

Liverpool wamekataa kulipa pesa iliyo kwenye mkataba wa mshambuliaji wa RB Leipzig Timo Werner 24, cha kiasi ya £50m, Majogoo hao wa Jiji la Liverpool wamemthaminisha strika huyo kwa kiasi cha £30.

Tottenham wanatazamia kuzipiku timu za EPL zinazowania saini ya winga wa FC Bournemouth na Scotland Ryan Fraser, 26.

Mabosi wa Ligi Kuu nchini England wameambiwa msimu unaweza ukamalizika ndani ya wiki sita tu kama mpango wa kuirejesha itaanza kama ilivyopangwa.

Author: Bruce Amani