Tetesi za Mastaa Ulaya: Paul Pogba asema hana furaha Manchester United

Kiungo mshambuliaji na ghali wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba amesema hana furaha na hali ambayo inaendelea klabuni hapo kwa kukosa muda wa kutosha kucheza ikiwa ni mara ya kwanza kukosa nafasi ndani ya Old Trafford huku tetesi zikidai kuwa Real Madrid na Juventus ziko macho kwa staa huyo.

Manchester City wameweka kipaumbele kwenye eneo la ushambuliaji katika dirisha kubwa la usajili la Juni 2021, mshambuliaji wa Borrusia Dortmund Erling Haaland 20 na Lautaro Martinez wanatajwa kuwa kwenye rada za klabu hiyo.

Hata hivyo City pia inafikiria kumnyakua kiungo wa Aston Villa Jack Glealish, 25, na Douglas Luiz, 25, wote wakitokea katika klabu ya Villa.

Chelsea wako tayari kumuuza kiungo wao mkabaji raia wa Ufaransa Tiemoue Bakayoko, 26, kwenda Napoli baada ya muda wa mkopo kumalizika mwishoni mwa msimu huu.

Beki wa Chelsea Antonio Rudiger, 27, huenda akajiunga na Barcelona katika dirisha dogo la usajili la mwezi Januari baada ya usajili wa Juni kushindikana kwa mpango huo.

Mkurugenzi wa Michezo wa Liverpool Michael Edwards amesema atafanya mazungumzo na Wakala wa mlinzi wa Napoli Kalidou Koulibaly, 29, kwa ajili ya kuangalia uwezekano wa kumsajili beki huyo wa kati wa Senegal.

Author: Asifiwe Mbembela