Tetesi za Mastaa Ulaya: PSG wataka Euro milioni 200 kwa PSG, Guardiola kuachana na Man City

Klabu ya Paris St-Germain imesema inahitaji kiasi cha pauni milioni 188 kwa ajili ya kumuuza winga wa kimataifa wa Ufaransa Kylian Mbappe, 22, klabu ya Real Madrid imeonyesha nia ya kumsajili winga huyo wa zamani wa Monaco.

Manchester City bado hawajakata tamaa ya kumsajili staa wa Juventus na Ureno Cristiano Ronaldo 36, ambaye ameonyesha nia ya kung’oka klabuni hapo, anaweza akawa mbadala wa Harry Kane ambaye amewekewa ngumu Spurs.

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola ataondoka klabuni hapo baada ya mkataba wake kumalizika klabuni hapo msimu wa 2022-23, baada ya kutoka klabuni hapo atapumzika.

Kocha wa Arsenal Mikel Arteta hayuko kwenye uhatari wa kupoteza nafasi ya kufukuzwa kazi klabuni hapo licha ya matokeo kuwa mabaya mwanzoni mwa Ligi, kocha wa zamani wa Chelsea Antonio Conte ameonyesha nia ya kusajiliwa.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares