Tetesi za Mastaa Ulaya: Real Madrid yajitoa kumsajili Kylian Mbappe, Barcelona yahitaji huduma ya beki wa Arsenal

Real Madrid wamejiondoa kwenye ushawishi wa kumsajili winga wa Kifaransa na Paris St-Germain Kylian Mbappe 22, baada ya kushindwa kukubaliana masuala ya kifedha.

Hata hivyo, klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu nchini Hispania La Liga imefikia makubaliano ya kumsajili kiungo wa Rennes Eduardo Camavinga, 18. Madrid walikuwa wanashindana na PSG na Manchester United. Camavinga ameichagua Madrid na kusajiliwa kwa euro milioni 31.
Barcelona watajaribu kumsajili beki wa kulia wa Arsenal na Hispania Hector Bellerin, 26, kama beki wa Brazil Emerson Royal, 22, ataondoka Nou Camp na kujiunga na Tottenham Hotspur.
Manchester City wamemaliza usajili kwa kuwatoa na kuwaingiza wachezaji kwenye timu kufuatia winga Bernardo Silva 26, amebakia sawa na kipa Ederson 28, kubakia pia kwa mkataba mpya.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares