Tetesi za Mastaa Ulaya: Renato Sanches awindwa na Barcelona, Ronaldo PSG ngumu kutokea

Juventus wanaangalia uwezekano wa kufanya uhamisho wa kiungo wa Paris St-Germain na Argentina Leandro Paredes, 27, hii ni baada ya kuumia kwa kiungo wa Kibrazil Arthur Melo, 24.

Barcelona wanavutiwa kumsajili kiungo mshambuliaji wa Lille na Ureno Renato Sanches, 23, thamani ya mchezaji huyo inatajwa kuwa pauni milioni 30.
Brighton wameonyesha nia ya kumsajili mshambuliaji wa Barcelona na Denmark Martin Braithwaite, 30, ambaye amekuwa akihusishwa pia na West Ham United na Wolves.
Cristiano Ronaldo huenda akalazimika kusalia kunako klabu ya Juventus kufuatia klabu hiyo kufuta uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina na Paris St-Germain Mauro Icardi, 28.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares