Tetesi za Mastaa Ulaya: Ronaldo ahusishwa kutua Paris St-Germain

116

Paris St-Germain wataangalia uwezekano wa kumsajili strika hatari wa Ureno na klabu ya Juventus Cristiano Ronaldo, 35, endapo miamba ya soka la Italia wataamua kumuuza. PSG wako kwenye mazungumzo na staa wa timu hiyo na Brazil Neymar Jr, 28, kwa ajili ya mkataba mpya wa miaka mitano.

Arsenal ni miongoni mwa vilabu vinavyowania saini ya mshambuliaji wa Sao Paulo Brenner, 20.

Mlinzi wa zamani wa Liverpool Jamie Carragher anaamini klabu ya Manchester United inatakiwa kumuuza kiungo wao ghali Paul Pogba, 27, kutokana na kushindwa kutoa kitu chema klabuni hapo kwa mwaka wa nne sasa.

Manchester United wanaweza kukamilisha uhamisho wa staa wa Aston Villa Jack Grealish, 25, endapo United wataamua kuachana na kiungo Paul Pogba.

Author: Bruce Amani